• HABARI MPYA

  Sunday, May 28, 2023

  LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE YA 4-4 NA SOUTHAMPTON


  TIMU ya Liverpool imekamilisha msimu wa Ligi Kuu ya England kwa sare ya mabao 4-4 na Southampton iliyoshuka daraja leo Uwanja wa St. Mary's Jijini Southampton, Hampshire.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota mawili, dakika ya 10 na 73, Roberto Firmino dakika ya 14 na Cody Gakpo dakika ya 72, wakati ya Southampton yamefungwa na James Ward-Prowse dakika ya 19, Kamaldeen Sulemana dakika ya 28 na 47 na Adam Armstrong dakika ya 64.
  Kwa matokeo hayo Liverpool inamaliza na pointi 67 nafasi ya tano, huku Southampton ikiipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu na pointi 25 nafasi ya mwisho, ya 20 ikiungana na Leicester City yenye pointi 34 na Leeds United pointi 31 kushuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE YA 4-4 NA SOUTHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top