• HABARI MPYA

  Friday, May 12, 2023

  SIMBA SC YAISHUSHA DARAJA RUVU SHOOTING, YAICHAPA 3-0 CHAMAZI


  WINGA Msenegal, Pape Ousmane Sakho ametokea benchi kipindi cha pili kuifungia Simba mabao mawili ikiichapa Ruvu Shooting 3-0 usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Matokeo hayo yanamaanisha Ruvu Shooting imeipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu kuelekea mechi mbili za mwisho, kwani pointi ilizonazo hata itashinda mechi zake mbili zilizosalia itamaliza nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16.
  Kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama aliifungia Simba bao la kwanza dakika ya 30, kabla ya Sakho kuongeza mawili dakika ya 72 na 90 na ushei.
  Simba SC inafikisha pointi 67 katika mchezo wa 28, nyuma ya Mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 71 za mechi 27 ambao wanaweza kutawazwa kuwa mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo kama watashinda dhidi ya Dodoma Jiji FC hapo hapo Chamazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAISHUSHA DARAJA RUVU SHOOTING, YAICHAPA 3-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top