• HABARI MPYA

  Thursday, May 25, 2023

  MAN CITY YAAMBUA SARE KWA BRIGHTON THE AMEX


  MABINGWA mara tatu mfululizo, Manchester City usiku wa jana wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa The AMEX, Falmer, East Sussex.
  Phil Foden alianza kuifungia Manchester City dakika ya 25, kabla ya Julio Enciso kuisawazishia Brighton & Hove Albion dakika ya 38.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City inafikisha pointi 89 pale juu sasa ikiizidi pointi nane Arsenal baada ya wote kucheza mechi 37, wakati Brighton imefikisha pointi 62 za mechi 37 pia nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAAMBUA SARE KWA BRIGHTON THE AMEX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top