• HABARI MPYA

  Wednesday, May 10, 2023

  WAZIRI WA MICHEZO AWAKABIDHI YANGA MAMILIONI YA RAIS SAMIA


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Hadhara Chana akimkabidhi Nahodha wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto Fedha Taslimu Sh. Milioni 20, zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini leo, Sh. Milioni 10 kila bao.
  Mabingwa hao wa Tanzania, Yanga SC wamebisha hodi Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na viungo marafiki, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 64 na Mghana Bernard Morrison dakika ya 90 na ushei na sasa wanatakiwa kwenda kuulinda ushindi huo kwenye mchezo wa marudiano Mei 17 Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng, NW.
  Wakiitoa Marumo, Yanga watakutana na mshindi wa jumla kati ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na USM Alger ya Algeria katika Fainali zitakazopigwa Mei 28 na Juni 3.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI WA MICHEZO AWAKABIDHI YANGA MAMILIONI YA RAIS SAMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top