• HABARI MPYA

  Sunday, May 28, 2023

  CHELSEA YAMALIZA LIGI KWA SARE YA 1-1 NA NEWCASTLE


  TIMU ya Chelsea imefunga msimu wa Ligi Kuu ya England kwa sare ya 1-1 na Newcastle United leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Newcastle United ilitangulia na bao la Anthony Gordon dakika ya tisa, kabla ya Kieran Trippier kujifunga kuisawazishia Chelsea dakika ya 27 baada ya kazi nzuri ya winga Raheem Sterling.
  Kwa matokeo hayo, Chelsea inamaliza na pointi 44 nafasi ya 12 na Newcastle United pointi 71 nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAMALIZA LIGI KWA SARE YA 1-1 NA NEWCASTLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top