• HABARI MPYA

  Thursday, May 11, 2023

  ROBERTINHO: NIMEONGEA NA WACHEZAJI TUSHINDE MECHI ZOTE ZILIZOSALIA MASHABIKI WAFURAHI


  KOCHA wa Simba SC, Mbrazil Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema kwamba wanahitaji kushinda mechi zote zilizosalia kwa heshima ya klabu ili wamalize na wastani mzuri wa pointi.
  Robertinho ameyasema katika mkutano na Waandishi wa Habari leo kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  “Jana nimeongea na wachezaji wangu kuhusu michezo hii iliyobaki na tupo tayari kuhakikisha tunashinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu,”amesema Robertinho.
  Simba SC inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ikiwa na pointi 64, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 71 baada ya wote kucheza mechi 27.
  Yanga inahitaji ushindi katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Dodoma Jiji FC hapo hapo Chamazi ili kutawazwa rasmi kuwa tena mabingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa pili mfululizo na mara ya 29 jumla. 
  Ikumbukwe Simba Jumapili ilitolewa katika Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kufuatia kuchapwa 2-1 na Azam FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Pamoja na hayo hata ikipoteza mechi zake zote zilizosalia bado itamaliza nafasi ya pili, ambayo inawapa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROBERTINHO: NIMEONGEA NA WACHEZAJI TUSHINDE MECHI ZOTE ZILIZOSALIA MASHABIKI WAFURAHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top