• HABARI MPYA

  Saturday, May 20, 2023

  AL AHLY WATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


  MABINGWA wa kihistoria, Al Ahly wamefanikiwa kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya sita katika misimu saba baada ya kuichapa Esperance ya Tunsia 1-0 usiku wa jana Jijini Cairo, Msri.
  Bao pekee la Al Ahly jana lilifungwa na Hussein Elshahat dakika ya 22 na kwa matokeo hayo wanakwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-0 baada ya kuichapa Esperance 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Tunisia.
  Mashetani hao Wekundu watasubiri mshindi kati ya mabingwa watetezi, Wydad Athletic Club na Mamelodi Sundowns zinazokutana katika mchezo wa marudiano leo mjini Pretoria, Afrika Kusini baada ya sare ya 0-0 kwenye mechi ya kwanza Casablanca.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY WATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top