• HABARI MPYA

  Sunday, May 21, 2023

  MAYELE AIPELEKA YANGA FAINALI ASFC


  MABINGWA watetezi, Yanga  wamekata tiketi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuwachapa wenyeji, Singida Big Stars 1-0 leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 82 akimalizia mpira uliookolewa na kipa Benedict Haule kufuatia shuti la winga mzawa, Dennis Nkane.
  Sasa Yanga ambao tayari wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa pili mfululizo, itakutana na Azam FC katika Fainali ya Azam Sports Federation Cup baadaye mwezi huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Yanga sasa wanarejea Dar es Salaam kuanza kujiandaa na Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Timu hizo zitarudiana Juni 3 Jijini Algiers nchini Algeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE AIPELEKA YANGA FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top