• HABARI MPYA

  Tuesday, May 16, 2023

  CURTIS JONES APIGA MBILI LIVERPOOL YAICHAPA LEICESTER 3-0


  TIMU ya Liverpool jana iliichapa Leicester City mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa King Power Jijini Leicester, Leicestershire.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Curtis Jones mawili dakika ya 33 na 36 mara zote akimalizia kazi nzuri za Mohamed Salah na la tatu akaweka kambani Trent Alexander-Arnold dakika ya 71.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 65 katika mchezo wa 36, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi moja na Manchester United ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi, wakati Leicester City inabaki na pointi zake 30za mechi 36 nafasi ya 19 mbele ya Southampton ambayo imekwishashuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CURTIS JONES APIGA MBILI LIVERPOOL YAICHAPA LEICESTER 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top