• HABARI MPYA

  Sunday, May 14, 2023

  MAN CITY YAIPIGA EVERTON 3-0 GOODISON PARK


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamejisogeza jirani mno na taji lingine la Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Everton leo Uwanja wa Goodison Park, Liverpool.
  Mabao ya Manchester City leo yamefungwa na Nahodha, Ilkay Gundogan mawili dakika ya 37 na 51 na Erling Haaland dakika ya 39, ambalo linakuwa bao lake la 36 msimu huu.
  Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 85 katika mchezo wa 35 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi nne zaidi ya Arsenal akihitaji kushinda mchezo ujao dhidi ya Chelsea Mei 21 kutawazwa rasmi kuwa bingwa tena.
  Kwa upande wao Everton baada ya kuchapwa leo wanabaki na pointi zao 32 za mechi 36 nafasi ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIPIGA EVERTON 3-0 GOODISON PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top