• HABARI MPYA

  Sunday, May 21, 2023

  NOTTINGHAM WAIPA UBINGWA MAN CITY...WAIPIGA ARSENAL 1-0

   

  TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya tatu mfululizo baada ya Arsenal jana kuchapwa 1-0 na Nottingham Forest Uwanja wa The City Ground, Nottingham, Nottinghamshire.
  Bao pekee la Nottingham Forest lilifungwa na mshambuliaji Mnigeria, Taiwo Micheal Awoniyi dakika ya 19 na sasa Manchester City ni mabingwa kwa sababu pointi zao 85 katika mechi 35 haziwezi tena kufikiwa na timu yoyote.
   Nottingham Forest wanafikisha pointi 37 katika mchezo wa 37, ingawa wanabaki nafasi ya 16, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 81 za mechi 37 nafasi ya pili, ambako hakuna wa kuwapita kutoka chini.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NOTTINGHAM WAIPA UBINGWA MAN CITY...WAIPIGA ARSENAL 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top