• HABARI MPYA

  Wednesday, May 10, 2023

  YANGA YANUSA FAINALI AFRIKA, YAICHAPA MARUMO GALLANTS 2-0 DAR


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wamebisha hodi Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, vijana wa kocha Mtunisia, Nasredeen Nabi wakaimaliza Marumo Gallants kipindi cha pili kwa mabao ya viungo marafiki, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 64 na Mghana Bernard Morrison dakika ya 90 na ushei.
  Sasa Yanga SC wanatakiwa kwenda kuulinda ushindi huo kwenye mchezo ww marudiano Mei 17 Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng, NW.
  Wakiitoa Marumo, Yanga watakutana na mshindi wa jumla kati ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na USM Alger ya Algeria katika Fainali zitakazopigwa Mei 28 na Juni 3.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YANUSA FAINALI AFRIKA, YAICHAPA MARUMO GALLANTS 2-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top