• HABARI MPYA

  Sunday, May 28, 2023

  MAN UNITED YAICHAPA FULHAM 2-1 DE GEA AOKOA PENALTI


  TIMU ya Manchester United imehitimisha msimu wa Ligi Kuu ya England kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na Jadon Sancho dakika ya 39 na Bruno Fernandes dakika ya 55 baada ya Fulham kutangulia na bao la Kenny Tete dakika ya 19, huku kipa David de Gea akiokoa mkwaju wa penalti wa Aleksandar Mitrovic dakika ya 26.
  Kwa ushindi huo, Manchester United inamaliza na pointi 75 nafasi ya tatu na Fulham inamaliza na pointi 52 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA FULHAM 2-1 DE GEA AOKOA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top