• HABARI MPYA

  Friday, May 12, 2023

  NABI: TUMEKUBALIANA NA VIJANA WAKAJITUME KESHO TUCHUKUE UBINGWA


  KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mtunisia Nasredeen Nabi amesema kwamba amewaambia wachezaji wake wakajitume washinde mechi ya kesho dhidi ya Dodoma Jiji ili watawazwe rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo.
  Nabi amesema hayo leo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jijini la Dar es Salaam.
  Yanga SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 71, ikifuatiwa na watani wao, Simba SC wenye pointi 64 kuelekea mechi tatu za mwisho.
  Lakini Yanga wanaweza kuanza kufurahia ubingwa hata leo iwapo Simba SC itapoteza mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao unaanza Saa 1:00 usiku hapo hapo Azam Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NABI: TUMEKUBALIANA NA VIJANA WAKAJITUME KESHO TUCHUKUE UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top