• HABARI MPYA

  Friday, May 12, 2023

  ROMA YATANGULIZA MGUU FAINALI EUROPA LEAGUE


  BAO pekee la Edoardo Bove dakika ya 62 limeipa ushindi stahiki AS Roma dhidi ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Europa League usiku wa Alhamisi Uwanja wa Olimpico Jijini Roma nchini Italia.
  Mechi nyingine ya kwanza ya Nusu Fainali ya Europa League bao la Federico Gatti dakika ya 90 na ushei liliinusu Juventus kufungwa nyumbani ikitoa sare ya 1-1 na Sevilla iliyotangulia na bao la Youssef En-Nesyri dakika ya 26 Uwanja wa Allianz Jijini Turin, Italia.
  Timu hizo zitarudiana Mei 18 na washindi watakutana katika Fainali Jumatano ya Mei 31 Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest nchini Hungary.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROMA YATANGULIZA MGUU FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top