• HABARI MPYA

  Saturday, May 13, 2023

  CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA NOTTINGHAM FOREST DARAJANI


  TIMU ya Nottingham Forest imetoka nyuma na kupata sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji, Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Nottingham Forest yamefungwa na mshambuliaji wake wa Kimataifa wa Nigeria, Taiwo Michael Awoniyi yote mawili, dakika ya 13 na 62, wakati ya Chelsea yamefungwa na nyota wa England, Raheem Sterling yote pia, dakika ya 51 na 58.
  Kwa sare huyo Chelsea inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 35 nafasi ya 11 na Nottingham Forest inafikisha pointi 34 za mechi 36 nafasi ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA NOTTINGHAM FOREST DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top