• HABARI MPYA

  Sunday, May 14, 2023

  YANGA SC WAIFUATA MARUMO GALLANTS KWA KAZI YA JUMATANO


  KIKOSI cha Yanga kimeondoka mapema leo asubuhi kwenda Afrika Kusini kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Gallants Gallants Jumatano.
  Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Uwanja wa Royal Bafokeng mjini, Phokeng Jijini Rustenburg nchini Afrika Kusini kuanzia Saa 1:00 usiku na kuonyeshwa LIVE na Televisheni ya ZBC 2.
  Yanga wanatakiwa kuulinda ushindi wao wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumatano iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mchezo mwingne wa marudiano wa Nusu Fainali utafuatia Saa 4:00 usiku Jumatano Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers kati ya wenyeji, USM Alger na ASEC Mimosas ambazo mechi ya kwanza zilitoka sare ya 0-0 Jumatano Uwanja wa Bouaké, Ivory Coast.
  Ikumbukwe Fainali za Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu zitachezwa Mei 28 na Juni 3.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAIFUATA MARUMO GALLANTS KWA KAZI YA JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top