• HABARI MPYA

  Monday, May 22, 2023

  WACHEZAJI SIMBA SC WAPEWA MAPUMZIKO TENA


  BENCHI la Ufundi la Simba SC limewapa mapumziko wachezaji wake hadi Jumatano kufuatia kusogezwa mbele kwa mechi mbili za mwisho za kumalizia msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  “Baada ya mchezo ujao wa Ligi Kuu kusogezwa hadi Juni 6, 2023, makocha wetu wametoa mapumziko kwa wachezaji na sasa watarudi kuendelea na mazoezi siku ya Jumatano Mei 24, 2023,” imesema taarifa ya Simba SC leo.
  Bodi ya Ligi imesogeza mbele mechi hizo ili kupisha michezo miwili ya Yanga ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Jumapili wiki hii Dar es Salaam na Juni 3 Jijini Algiers.
  Sasa mechi hizo za kumalizia msimu zitachezwa Juni 6 na Juni 9 na baada ya hapo itafuatia Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu Azam Sports Federation Cup (ASFC) katí ya Azam FC na Yanga Jijini Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WACHEZAJI SIMBA SC WAPEWA MAPUMZIKO TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top