• HABARI MPYA

  Sunday, May 28, 2023

  YANGA YAJIWEKA PAGUMU FAINALI SHIRIKISHO, YACHAPWA 2-1 NYUMBANI


  TIMU ya Yanga imeshindwa kutumia vizuri Uwanja wa nyumbani, Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam baada ya kufungwa mabao 2-1 na USM Alger katika mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Mabao ya USM Alger yamefungwa na mshambuliaji Aimen Mahious dakika ya 32 na kiungo Islam Merili dakika ya 84, wakati la Yanga limefungwa na mshambuliaji wake Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 82.
  Sasa Yanga wanakabiliwa na mtihani mgumu we kwenda kushinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers Jumapili ijayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAJIWEKA PAGUMU FAINALI SHIRIKISHO, YACHAPWA 2-1 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top