• HABARI MPYA

  Sunday, May 14, 2023

  ARSENAL YACHAKAZWA 3-0 NA BRIGHTON PALE PALE EMIRATES  NDOTO za Arsenal FC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England zimeyeyuka rasmi leo baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Brighton & Hove Albion FC leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Brighton & Hove Albion yamefungwa na Julio Enciso dakika ya 51, Deniz Undav dakika ya 86 na Pervis Estupiñán dakika ya 90.
  Ushindi huo unaifanya Brighton ifikishe pointi 58 katika mchezo wa 34 na kusogea nafasi ya sita, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 81 za mechi 36 nafasi ya pili.
  Hii maana yake, Manchester City yenye pointi 85 za mechi 35 inahitaji kushinda mechi moja zaidi ili kutawazwa tena kuwa mabingwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YACHAKAZWA 3-0 NA BRIGHTON PALE PALE EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top