• HABARI MPYA

  Saturday, May 27, 2023

  UWANJA WA BENJAMIN MKAPA TAYARI UMEFURIKA YANGA V USM ALGER


  TIKETI zote 60,000 za madaraja tofauti ya mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Yanga na USM Alger ya Algeria kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam zimeuzwa.
  Maana yake Uwanja umekwishasheheni Saa 30 na ushei kabla ya mchezo wenyewe, ambao utafuatiwa mechi ya marudiano Juni 3 Jijini Algiers Julai 5, 1962 Jijini Algiers.
  Mechi hiyo itachezeshwa na refa, Jean-Jacques Ngambo Ndala atakayesaidiwa na Olivier Kabene Safar wote kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zakhele Thusi Granville Siwela wa Afrika Kusini watakaokuwa wanakimbia na vibendera pembezoni mwa Uwanja kulia na kushoto.
  Kufika hatua hii, Yanga iliitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini, wakati USM Alger iliitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UWANJA WA BENJAMIN MKAPA TAYARI UMEFURIKA YANGA V USM ALGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top