• HABARI MPYA

  Saturday, May 20, 2023

  WYDAD YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA


  MABINGWA watetezi, Wydad Athletic Club wametoka nyuma mara mbili kupata sare ya 2-2 na wenyeji, Mamelodi Sundowns katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria, Afrika Kusini.
  Mabao ya Mamelodi Sundown yamefungwa na Themba Zwane dakika ya 50 na Mnamibia Peter Shalulile dakika ya 79, wakati ya Wydad yamefungwa na Ayoub El Amloud dakika ya 72 na Mothobi Mvala aliyejifunga dakika ya 83.
  Kwa matokeo hayo, Wydad inanufaika na mabao ya ugenini baada ya sare ya awali nyumbani ya bila kufungana Jijini Casablanca nchini Morocco.
  Watakutana na mabingwa wa kihistoria, Al Ahly ya Misri katika marudio ya Fainali ya msimu uliopita.
  Al Ahly imeitoa Esperance ya Tunisia kwa jumla ya mabao 4-0, ikishinda 3-0 ugenini na 1-0 nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WYDAD YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top