• HABARI MPYA

  Tuesday, May 23, 2023

  DENVER NUGGETS WASHINDI WA NBA WESTERN CONFERENCE


  TIMU ya Denver Nuggets imeingia Fainali za Ligi ya mpira wa Kikapu Marekani (NBA) kwa mara ya kwanza katika historia yao baada ya ushindi wa pointi 113-111 dhidi ya Los Angeles Lakers kwenye Fainali ya Western Conference Alfajiri ya leo.
  Pongezi kwa Nikola Jokic aliyefunga pointi 30, rebounds 14 na assists 13 na kuivusha Denver Nuggets kwa ushindi wa jumla ya Series 4-0.
  Mfungaji Bora wa muda wote wa NBA, LeBron James akiwa katika mechi ya mwisho msimu wake wa 20 kwenye histora yake ya NBA amejiwekea rekodi binafsi kwa kufunga pointi 31 kwenye first half ya Game 4.
  Mwamba huyo mwenye umri wa miaka 38, James kwa ujumla amefunga pointi 40, rebounds 10, assists tisa ingawa haikumsaidia Mfungaji huyo Bora wa muda wote wa NBA kuinusuru Lakers na kipigo cha nne mfululizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DENVER NUGGETS WASHINDI WA NBA WESTERN CONFERENCE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top