• HABARI MPYA

  Wednesday, May 17, 2023

  JKT QUEENS MABINGWA LIGI YA WANAWAKE TANZANIA BARA


  TIMU ya JKT Tanzania imefanikitwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa Mkwawa Queens leo Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Wapinzani wao wakuu katika mbio za ubingwa na waliokuwa mabingwa pia, Simba Queens ambao leo wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Ceasiaa Queens Uwanja wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mjini Iringa pia.
  Kwa matokeo hayo, JKT Queens inamaliza na pointi 46, moja zaidi ya Simba Queens, wakati Fountain Gate Princess iliyomaliza na pointi 41 imeshika nafasi ya tatu na Yanga Princess yenye pointi 34 ni ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT QUEENS MABINGWA LIGI YA WANAWAKE TANZANIA BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top