• HABARI MPYA

  Sunday, May 14, 2023

  NAMUNGO YAILAZA AZAM FC 2-1 PALE PALE CHAMAZI


  TIMU ya Namungo FC imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya wenyeji, Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Azam FC ilitangulia kwa bao la kujifunga la beki kutoka Benín, Pertene Counou dakika ya 19, kabla ya Namungo kuzinduka kwa mabao ya Hassan Kabunda dakika ya 25 na Shiza Kichuya dakika ya 54.
  Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 39 na kusogea nafasi ya tano, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 53 nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO YAILAZA AZAM FC 2-1 PALE PALE CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top