• HABARI MPYA

  Friday, May 26, 2023

  MAN UNITED YAICHAPA CHELSEA 4-1 NA KUFUZU LIGI YA MABINGWA


  TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Chelsea kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na Carlos Casemiro dakika ya sita, Anthony Martial dakika ya 45 na ushei, Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya 73 na Marcus Rashford dakika ya 78, wakati la Chelsea limefungwa na João Félix dakika ya 89.
  Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 72 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi pointi mbili Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 37.
  Ni matokeo ambayo yanaihakikishia Manchester United kurejea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, ambao ni mwanzo mzuri kwa kocha Mholanzi, Erik ten Hag kwenye msimu wake wa kwanza.
  Kwa upande wao Chelsea kipigo hicho kinawaacha na pointi zile zile 43 za mechi 37 pia nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA CHELSEA 4-1 NA KUFUZU LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top