• HABARI MPYA

  Friday, May 12, 2023

  YANGA YAINGIA MKATABA NA ROBBIALAC KUING’ARISHA JANGWANI


  KLABU ya Yanga leo imeitangaza kampuni ya Berger inayotengeneza rangi za Robbialac kuwa mshirika wake ambaye atafanya kazi ya kupaka rangi jengo lao la Makao Makuu, Jangwani, Dar es Salaam.
  Katika hatua nyingine kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka Jumapili kwenda Rusternburg, Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Marumo Gallants Jumatano Uwanja wa Royal Bafokeng.
  Yanga itakwenda huko ikihitaji kuulinda ushindi wake wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumatano Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAINGIA MKATABA NA ROBBIALAC KUING’ARISHA JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top