• HABARI MPYA

  Friday, May 12, 2023

  KMC YAICHAPA SINGIDA BIG STARS 2-0 UHURU


  TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC yamefungwa na Daruwesh Saliboko dakika ya 20 na Cliff Buyoya dakika ya 84 na kwa ushindi huo wakicheza mechi ya pili chini ya kocha mpya, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ wanafikisha pointi 29 na kusogea nafasi ya 12, 
  Kwa upande wao Singida Big Stars walio chini ya kocha Mholanzi, Hans van Pluijm wanabaki na pointi zao 51 nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAICHAPA SINGIDA BIG STARS 2-0 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top