• HABARI MPYA

  Thursday, May 18, 2023

  FAINALI YANGA ITAANZIA NYUMBANI MEI 28 MARUDIANO JUNI 3 ALGERIA


  TIMU ya Yanga itaanzia nyumbani katika Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Mei 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Algeria kwa mchezo wa marudiano Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.
  USM Alger imeitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani, wakati Yanga imeitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FAINALI YANGA ITAANZIA NYUMBANI MEI 28 MARUDIANO JUNI 3 ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top