• HABARI MPYA

  Monday, May 22, 2023

  REFA WA JUMAPILI YANGA NA USM ALGER NI MKONGO


  REFA kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean-Jacques Ngambo Ndala ndiye atakayechezesha Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili wiki hii Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Ngambo Ndala atasaidiwa na Mkongo mwenzake Olivier Kabene Safar na Zakhele Thusi Granville Siwela wa Afrika Kusini watakaokuwa wanakimbia na vibendera pembezoni mwa Uwanja kulia na kushoto.
  Mchezo wa marudiano utafuatia Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litatoa orodha nyingine ya waamuzi.
  Kufika hatua hii, Yanga imeitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini, wakati USM Alger imeitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA WA JUMAPILI YANGA NA USM ALGER NI MKONGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top