• HABARI MPYA

  Saturday, May 13, 2023

  YANGA BINGWA TENA LIGI KUU, YAICHAPA DODOMA JIJI 4-2 CHAMAZI


  YANGA SC ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo kufuatia ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Dodoma Jiji leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Haukuwa ushindi mwepesi, kwani pamoja na Yanga kutangulia kwa bao la mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda dakika ya 39, lakini kipindi cha pili Dodoma Jiji walitoka nyuma na kuongoza 2-1 hadi dakika ya 70.
  Collins Okpare aliisawazishia Dodoma Jiji dakika ya 59 na SEIF Abdallah Karihe akafunga la pili dakika ya 67, kabla ya Mudathir Yahya kuisawazishia Yanga dakika ya 70.
  Mabao mawili ya ushindi ya Yanga yalifungwa na Farid Mussa dakika ya 88 na Mudathir Yahya dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 74 ambazo zinawahakishia ubingwa, kwani hata wakipoteza mechi mbili zilizosalia na mtani Simba hata akishinda zote mbili bado wataendelea kuongoza.
  Katika mchezo wa leo, Dodoma Jiji ilimaliza pungufu baada ya Mbwana Kibuta kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 72 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumghasi refa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA BINGWA TENA LIGI KUU, YAICHAPA DODOMA JIJI 4-2 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top