• HABARI MPYA

  Thursday, May 18, 2023

  MANCHESTER CITY WAITANDIKA REAL MADRID 4-0 ETIHAD


  WENYEJI, Manchester City wametinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhdiyya waliokuwa mabingwa watetezi, Real Madrid usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Shujaa wa Manchester City usiku huo alikuwa na ni kiungo Mreno, Bernardo Silva aliyefunga mabao mawili dakika ya 23 na 37, wakati mengine yamefungwa na beki Mswisi, Manuel Obafemi Akanji dakika ya 76 na mshambuliaji Muargentina, Julián Álvarez dakika ya 90.
  Sasa Manchester City wanakwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-1 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa Kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
  Manchester City watakutana na Inter Milán ya Italia katika Fainali Juni 10 Uwanja wa Atatürk Olimpiyat Jijini İstanbul nchini Uturuki.
  Inter Milán imefika Fainali baada ya kuwatoa mahasimu wao wa nyumbani, AC Milan kwa jumla ya mabao 3-0, wakishinda 2-0 na 1-0 Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milán.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY WAITANDIKA REAL MADRID 4-0 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top