• HABARI MPYA

  Tuesday, May 23, 2023

  MTANZANIA MADINA IDDI ASHINDA MASHINDANO YA GOFU KENYA


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Chana ametoa pongezi kwa Mtanzania, Madina Iddi kwa kuibuka wa kwanza katika mashindano ya Gofu ya Muthaiga Ladies Open 2023 yaliyomalizika hivi karibuni nchini Kenya. 
  Mhe. Chana ametoa pongezi hizo Mei 21, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akifunga  Mashindano ya Gofu ya Lugalo Ladies Open 2023, ambapo  ametoa Rai kwa Wanawake wajitokeze kwa wingi kushiriki michezo mbalimbali hususani mchezo wa Gofu kwa kuwa katika dunia ya sasa michezo inatoa fursa ya ajira.
  "Nalipongeza JWTZ na Klabu ya Gofu Lugalo kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi kutumia Klabu hii katika kuendeleza vipaji vyao na kukuza mchezo wa Gofu ambao unaendelea kukua siku hadi siku" amesema Mhe. Chana.
  Awali Mwenyekiti wa Lugalo Gofu Club Brigedia  Jenerali  Mstaafu, Michael Luwongo  amesema mashindano hayo yameshirikisha wanamichezo takriban 100 ambapo Wanawake ni zaidi ya 50.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTANZANIA MADINA IDDI ASHINDA MASHINDANO YA GOFU KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top