• HABARI MPYA

  Tuesday, May 09, 2023

  NABI: MECHI YA KESHO INAHITAJI AKILI NYINGI NA TAHADHARI KUBWA

  KOCHA Mtunisa wa Yanga, Nasredeen Nabi amesema kwamba mechi ya kesho dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini inahitaji akili na tahadhari kubwa sana ili kupata matokeo mazuri.
  Yanga SC watakuwa wenyeji wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kesho katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kunzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Timu hizo zitarudiana Mei 17 Uwanja wa Venue Royal Bafokeng, Phokeng, NW na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na USM Alger ya Algeria katika Fainali zitakazopigwa Mei 28 na Juni 3.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NABI: MECHI YA KESHO INAHITAJI AKILI NYINGI NA TAHADHARI KUBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top