• HABARI MPYA

  Saturday, May 13, 2023

  KITAYOSCE YA TABORA YAPANDA LIGI KUU, PAMBA KUJARIBU ‘MLANGO WA UANI’


  TIMU ya Kitayosce FC imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Sports ya Tanga leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora.
  Kitayosce imefikisha pointi 60, moja zaidi ya Pamba FC ambayo pia leo imeshinda 2-1 dhidi ya Fountain Gate Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Kitayosce imeungana na JKT Tanzania, mabingwa wa Championship waliomaliza na pointi 63.
  Pamba itakwenda kumenyana na Mashujaa iliyomaliza na pointi 49 nafasi ya nne na mshindi wa jumla atakwenda kumenyana na timu iliyoporomoka kutoka Ligi Kuu kuwania kupanda.
  Mechi nyingine za mwisho za Championship leo, Green Warriors imeichapa Pan Africans 3-2, Mashujaa imeichapa Mbuni 2-1, Ken Gold imeichapa Biashara United 3-2 na Mbeya Kwanza imeichapa Copco FC 4-3.
  Gwambina na Ndanda FC zilizojitoa ndio zimeshuka, wakati Copco, Green Warriors, Pan African na Africans Sports zitakwenda kwenye mchujo wa kuwania kubaki Championship.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KITAYOSCE YA TABORA YAPANDA LIGI KUU, PAMBA KUJARIBU ‘MLANGO WA UANI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top