• HABARI MPYA

  Thursday, May 11, 2023

  CHINA WA YANGA SC ALIPOKUWA MCHEZAJI CHIPUKIZI LIGI KUU 1988


  WAZIRI Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba akimkabidhi Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi Ligi Kuu mwaka 1988, kiungo wa Yanga, Athumani Abdallah China. Katika sherehe hizo zilizohuhudhuriwa na viongozi wengine wa chama (CCM) na Serikali wakiwemo Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (sasa marehemu), Alhaji Mohamed Mussa na Fatuma Said Ally - Mheshimiwa Warioba pia alimkabidhi beki wa Reli, John Simkoko tuzo ya Mchezaji Mwenye umri mkubwa kuliko wote (miaka 40).
  Katika msimu huo, Coastal Union ya Tanga iliibuka bingwa baada ya kuizidi tu wastani wa mabao Yanga, huku Simba ikinusurika kushuka daraja baada ya kumaliza juu ya Tukuyu Stars ya Mbeya na Reli ya Morogoro zilizoteremka daraja.
  Ni ushindi wa 2-1 dhidi ya Yanga Julai 23, mwaka 1988 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru ndio uliowanusuru Simba kushuka daraja na kumaliza na pointi 20, mbili zaidi ya Tukuyu Stars. Siku hiyo mabao ya Simba yalifungwa na Edward Chumila dakika ya 21 na John Makelele dakika 58, wakati la Yanga lilifungwa na Issa Athumani dakika 36. Wafungaji wote wamekwishafariki dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHINA WA YANGA SC ALIPOKUWA MCHEZAJI CHIPUKIZI LIGI KUU 1988 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top