• HABARI MPYA

  Sunday, May 28, 2023

  NDOTO ZA PAMBA KUREJEA LIGI ZAYEYUKA, MASHUJAA WASONGA MBELE


  NDOTO za Pamba ya Mwanza kurejea Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mara nyingine zimeyeyuka licha ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Mashujaa ya Kigoma leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Mashujaa inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-4 kufuatia kuichapa Pamba 4-0 kwenye mchezo wa kwanza Kigoma na itamenyana na timu itakayoporomoka kutoka Ligi Kuu kuwania kupanda.
  Timu mbili za Ligi Kuu, ya 16 na ya 15 zitashuka moja kwa moja na zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao nyumbani na ugenini na itakayofungwa ndio itakwenda kucheza na Mashujaa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDOTO ZA PAMBA KUREJEA LIGI ZAYEYUKA, MASHUJAA WASONGA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top