• HABARI MPYA

  Saturday, May 27, 2023

  KACHUMBARI ALIYEWIKA SMALL SIMBA, MLANDEGE NA MALINDI AFARIKI DUNIA

  ALIYEWAHI kuwa beki wa timu za Kikwajuni, Small Simba, Mlandege, Malindi SC na Mafunzo, zote za Zanzibar, Mohamed Kachumbari (pichani kushoto) amefariki dunia asubuhi ya leo Jijini Dar es Salam.
  Taarifa za watu wa karibu wa marehemu zimesema, mwili wake umesafirishwa mchana wa leo kutoka Dar kwenda nyumbani kwao, Mwanakwerekwe Zanzibar kwa mazishi.
  Pamoja na Kikwajuni, Small Simba, Mlandege, Malindi SC na Mafunzo, marehemu Kachumbari pia alichezra timu ya taifa ya Zanzibar, 'Zanzibar Heroes' na ya Tanzania, 'Taifa Stars'.
  Mungu ampumzishe kwa amani. Amin.


  Mohamed Kachumbari, wa tatu kutoka kuliawaliosimama akiwa na kikosi cha Small Simba ya Zanzibar mwaka 1991 Jijini Mbabane, Swaziland (sasa Ewatini) kabla ya mechi ya marudiano Raundi ya Awali Kombe la Washindi Afrika dhidi ya wenyeji, Highlanders. 
  Wengine kulia ni Meneja, Hussein Lee na kipa Ridhaa Hamisi. Kushoto kwa Kachumbari ni Duwa Said, Karume Mussa, Ubwa Makame 'Mzungu', Innocent Haule, Rashid Hamisi na Hamisi Mpemba.
  Waliochuchumaa kutoka kulia ni Hajji Mwinyi, Gharib Mahmoud 'Latto', Juma Bakari 'Kidishi', Ally Diego, Issa Lambo, Zuberi Wambura, Khamis Abofu na Hamisi Kisaka. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KACHUMBARI ALIYEWIKA SMALL SIMBA, MLANDEGE NA MALINDI AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top