• HABARI MPYA

  Monday, March 27, 2023

  CAF YAAFIKI STARS NA CRANES ICHEZWE SAA 2:00 USIKU MKAPA

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeridhia mechi baina ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya Uganda, The Cranes ichezwe Saa 2:00 usiku kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Taifa Stars watakuwa wenyeji wa The Cranes kesho katika mchezo wa Kundi F kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ikihitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu.
  Taifa Stars itaingia dimbani na kumbukumbu ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda Ijumaa Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri, bao pekee la Simon Msuva.
  Kwa sasa Taifa Stars inashika nafasi ya pili Kundi F kwa pointi zake nne, nyuma ya Algeria yenye pointi tisa na mbele ya Niger yenye pointi mbili na Uganda pointi moja baada ya mechi tatu za awali.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAAFIKI STARS NA CRANES ICHEZWE SAA 2:00 USIKU MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top