• HABARI MPYA

  Tuesday, March 28, 2023

  SIMBA SC YAIFUATA RAJA KWA MAFUNGU MOROCCO


  KUNDI la kwanza la kikosi cha Simba SC linatarajiwa kuondoka leo kwenda Morocco kwa ajili ya mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Raja Casablanca Aprili 1 Uwanja wa Mfalme Mohamed V Jijini Casablanca.
  Tayari Simba SC imefuzu Robo Fainali Ligi ya Mabingwa baada ya kujikusanyia pointi tisa, nyuma ya vinara, Raja Casablanca, wakati Horoya yenye pointi nne na Vipers mbili zitakamilisha ratiba kwa mchezo baina yao Jijini Conakry Machi 31.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIFUATA RAJA KWA MAFUNGU MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top