• HABARI MPYA

  Sunday, March 19, 2023

  YANGA YAICHAPA MONASTIR 2-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI CAF


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastirienne katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshambuliaji Mzambia Kennedy Musonda aliifungia Yanga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 33 akimalizia krosi ya winga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jesús Moloko kutoka upande wa kulia wa Uwanja.
  Musonda akamsetia mshambuliaji wa Kimataifa wa DRC na kinara wa mabao wa klabu kwa msimu wa pili mfululizo kuifungia Yanga bao la pili dakika ya 59.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 10 na kupanda kileleni mwa Kundi D, ikiizidi tu wastani wa mabao US Monastirienne na zote zinafuzu Robo Fainali dhidi ya Real Bamako ya Mali na TP Mazembe ya DRC.
  Mechi nyingine ya Kundi D leo, wenyeji Real Bamako wameshinda 2-1 dhidi ya TP Mazembe Jijini Bamako nchini Mali.
  Sasa Real Bamako inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake tano na Mazembe inashika mkia kwa pointi zake tatu.
  Mechi za mwisho Yanga watakuwa wageni wa Mazembe Jijini Lubumbashi na Monastir watawakaribisha Real Bamako Jijini Tunis Aprili 2.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA MONASTIR 2-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top