• HABARI MPYA

  Friday, March 24, 2023

  MESSI AFUNGA BAO LA 800 ARGENTINA YASHINDA 2-0

  NAHODHA Lionel Messi jana amefunga bao lake la 800 katika ushindi wa 2-0 wa Argentina dhidi ya Panama kwenye mchezo wa kirafiki Uwanja wa Mâs Monumental, Capital Federal, Ciudad de Buenos Aires.
  Messi aliyekuwa anacheza timu ya taifa kwa mara ya kwanza tangu aipe Kombe la Dunia Desemba mwaka nchini Qatar alifunga bao lake kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 89 kufuatia Thiago Almada kufunga la kwanza dakika ya 78.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AFUNGA BAO LA 800 ARGENTINA YASHINDA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top