• HABARI MPYA

  Sunday, March 26, 2023

  SINGIDA BIG STARS YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI

  TIMU ya Singida Big Stars imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Dodoma ilitangulia kwa bao la Raizin Hafidh, kabla ya beki Nickson Kibabage kuisawazishia Singida Big Stars na yeye mwenyewe kufunga la pili.
  Ulikuwa mchezo maalum kwa timu zote kujipanga kwa hatia iliyobaki ya Ligi Kuu, lakini kwa Singida Jiji kujiandaa pia na Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top