• HABARI MPYA

  Saturday, March 25, 2023

  MAHODHA MPYA MBAPPE APIGA MBILI UFARANSA YAICHAPA UHOLANZI 4-0


  NAHODHA mpya, Kylian Mbappe usiku wa jana amefunga mabao mawili Stade de France mjini Saint-Denis kuiwezesha Ufaransa kuitandika Uholanzi 4-0 katika mchezo wa kwanza wa Kundi B kufuzu Euro 2024 Ujerumani.
  Mbappe ambaye pia ni Nahodha wa Paris Saint-Germain alifunga mabao yake dakika ya 21 na 88, wakati mabao mengine yamefungwa na Antoine Griezmann dakika ya pili na Dayot Upamecano dakika ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAHODHA MPYA MBAPPE APIGA MBILI UFARANSA YAICHAPA UHOLANZI 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top