• HABARI MPYA

    Thursday, March 30, 2023

    MWENZA WA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI ATEMBELEA JK PARK


    MWENZA wa Makamu wa Rais wa Marekani Mhe.Kamalla Haris Bw. Douglas Emhoff leo Machi 30, 2023 ametembelea Kituo Cha kukuza Vipaji vya Michezo Jakaya Kikwete Youth  Park kilichopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
    Katika zira hiyo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameshiriki pamoja na Mwenza wa Makamu wa Rais wa Marekani, Emhoff na kupata fursa ya kufanya ziara fupi kuona jinsi kituo hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuzungumza na vijana wanaofundishwa mpira wa Miguu na Kikapu katika Kituo hicho.
    Emhoff amewasihi vijana hao wajifunze kwa Ari na Bidii  ili waje kuwa nyota wazuri na wakubwa Duniani.
    Kwa upande wake Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana amemshukuru Mwenza huyo kwa ziara yake katika Kituo hicho ambapo amesema ni miongoni mwa vituo  vinavyolea  vipaji ambavyo vinatarajiwa kuisaidia nchi katika Sekta ya michezo.
    Balozi Dkt. Pindi Chana amesema  kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefungua milango kwa wadau ndani na nje ya nchi kuona fursa zilizopo nchini katika Sekta za Michezo, Utamaduni na Sanaa na kuzitumia katika kuleta maendeleo kwa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWENZA WA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI ATEMBELEA JK PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top