• HABARI MPYA

  Wednesday, March 29, 2023

  MESSI APIGA HAT TRICK KUFIKISHA MABAO 100 ARGENTINA

  NAHODHA Lionel Messi usiku wa kuamkia leo amefunga mabao matatu Argentina ikiibuka na ushindi wa 7-0 dhidi ya Curaçao katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Único Madre de Ciudades Jijini Santiago del Estero, Prov. de Santiago del Estero.
  Messi alifunga dakika za 20, 33 na 37, wakati mengine yamefungwa na Nicolás Iván González dakika ya 23, Enzo Jeremías Fernández dakika ya 35, Ángel Di María dakika ya 78 na Gonzalo Montiel dakika ya 87.
  Mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain  - ambaye wiki iliyopita alifikisha mabao 800 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Panama, sasa ametimiza mabao 100 ya kuifungia timu yake ya taifa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI APIGA HAT TRICK KUFIKISHA MABAO 100 ARGENTINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top