• HABARI MPYA

  Tuesday, March 21, 2023

  AZAM FC WAFUTA SAFARI YA KENYA SABABU YA MACHAFUKO


  KLABU ya Azam FC imesitisha safari yake ya Kenya kwenda kucheza na Gor Mahia Jumapili hii, kutokana na sababu za kiusalama.
  Azam FC, mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Kombe la Kagame, walialikwa na wababe hao wa Kenya, Gor Mahia kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki uliopangwa kufanyika Uwanja wa Nyayo Jijini Nairobi.
  Hata hivyo, mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar utafanyika kama ilivyopangwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex saa 1.00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WAFUTA SAFARI YA KENYA SABABU YA MACHAFUKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top