SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetambulisha jezi mpya za timu ya taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo kwa mashabiki watanunua kwa Sh. 45,000 kila moja.
Taifa Stars itakuwa na mechi mbili za ugenini na nyumbani za Kundi F kufuzu AFCON dhidi ya Uganda, mchezo wa kwanza Machi 24 Jijini Cairo nchini Misri na marudiano Machi 28 Dar es Salaam.
Taifa Stars itaingia kwenye mechi hizo ikiwa chini ya kocha mpya, Mualgeria mwenye uraia wa Ubelgiji, Adel Amrouche.
0 comments:
Post a Comment