• HABARI MPYA

  Tuesday, March 21, 2023

  DESCHAMPS AMTEUA MBAPPE KUWA NAHODHA MPYA UFARANSA


  KOCHA wa Ufaransa, Didier Deschamps amemteu Kylian Mbappe kuwa Nahodha mpya wa timu yake ya taifa.
  Uteuzi huo unakuja kuelekea mechi ya kufuzu Euro 2024 dhidi ya Uholanzi baada ya kujiuzulu kwa kipa Hugo Lloris kufuatia Fainali za Kombe la Dunia Ijumaa pale Stade de France.
  Nahodha wa zamani, Lloris alijiuzulu soka ya kimataifa baada ya Ufaransa kufungwa kwa penalti 4-2 na Argentina kwenye Fainali ya Kombe la Dunia Qatar Desemba 18 kufuatia sare ya 3-3.
  Tayari Mbappe amepewa Unahodha wa klabu yake, PSG na bila shaka hiyo imemsukuma Deschamps kumpa jukumu hilo na timu ya taifa, ingawa awali ilielezwa angemteua kipa wa AC Milan, Mike Maignan. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DESCHAMPS AMTEUA MBAPPE KUWA NAHODHA MPYA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top