• HABARI MPYA

  Wednesday, March 29, 2023

  MCTOMINAY APIGA MBILI SCOTLAND YAICHAPA HISPANIA 2-0


  KIUNGO wa Manchester United, Scott McTominay jana alifunga mabao yote mawili dakika ya saba na 51 kuiwezesha Scotland kushinda 2-0 dhidi ya Hispania Uwanja wa Hampden Park Jijini Glasgow katika mchezo wa Kundi A kufuzu Euro ya mwakani Ujerumani.
  McTominay anafikisha mabao manne ndani ya mechi mbili tu za mwanzo za Kundi A kufuzu Euro baada ya kuwafunga pia na Cyprus katika ushindi wa 3-0 kwenye mechi ya kwanza.
  Hii ni mara ya kwanza kwa Scotland kuifunga Hispania tangu mwaka 1984.
  Kwa Hispania hii ni mechi ya nane tu ya kufuzu wanafungwa kihistoria, iwe kwenye Kombe la Ulaya au Kombe la Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCTOMINAY APIGA MBILI SCOTLAND YAICHAPA HISPANIA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top